Psalms 25

Kumwomba Mungu Uongozi Na Ulinzi

(Zaburi Ya Daudi)


1
Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
bKwako wewe, Ee Bwana,
nainua nafsi yangu,

2 cni wewe ninayekutumainia,
Ee Mungu wangu.
Usiniache niaibike,
wala usiache adui zangu wakanishinda.

3 dKamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea
atakayeaibishwa,
bali wataaibishwa
wafanyao hila bila sababu.


4 eNionyeshe njia zako, Ee Bwana,
nifundishe mapito yako,

5 fniongoze katika kweli yako na kunifundisha,
kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu,
nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.

6 gKumbuka, Ee Bwana, rehema zako kuu na upendo,
kwa maana zimekuwepo tangu zamani.

7 hUsizikumbuke dhambi za ujana wangu
wala njia zangu za uasi,
sawasawa na upendo wako unikumbuke,
kwa maana wewe ni mwema, Ee Bwana.


8 i Bwana ni mwema na mwenye adili,
kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake.

9 jHuwaongoza wanyenyekevu katika haki,
naye huwafundisha njia yake.

10 kNjia zote za Bwana ni za upendo na uaminifu
kwa wale wanaoshika shuhuda za agano lake.

11 lEe Bwana, kwa ajili ya jina lako,
unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi.

12 mNi nani basi, mtu yule anayemcha Bwana?
Atamfundisha katika njia
atakayoichagua kwa ajili yake.

13 nMtu huyo atafanikiwa maishani mwake,
nao wazao wake watairithi nchi.

14 oSiri ya Bwana iko kwa wale wamchao,
yeye huwajulisha agano lake.

15 pMacho yangu humwelekea Bwana daima,
kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa
miguu yangu kutoka mtego.


16 qNigeukie na unihurumie,
kwa maana mimi ni mpweke na mwenye kuteseka.

17 rShida za moyo wangu zimeongezeka,
niokoe katika dhiki yangu.

18 sUangalie mateso na shida zangu
na uniondolee dhambi zangu zote.

19 tTazama adui zangu walivyo wengi,
pia uone jinsi wanavyonichukia vikali!

20 uUyalinde maisha yangu na uniokoe,
usiniache niaibike,
kwa maana nimekukimbilia wewe.

21 vUadilifu na uaminifu vinilinde,
kwa sababu tumaini langu ni kwako.


22 wEe Mungu, wakomboe Israeli,
katika shida zao zote!
Copyright information for SwhKC